Thursday, July 30, 2015

Rais wa Uefa Michael Platini mwenye miaka 60 ameshambuliwa kwa maneno na wagombea wenzake wawili masaa kadhaa tu tangu atangaze kuwania mikoba ya rais wa FIFA, Sepp Blatter jumatanohii.
Platini anasema FIFA inahitaji mabadiliko baada ya kugubikwa na skendo za rushwa.Lakini katika hali isiyotegemewa, aliyekuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi uliopita Prince Ali Bin-Hussein anayegombea tena hivi sasa anasema Platini sio mbadala sahihi wa Blatter na kwamba shirikisho hilo linamhitaji mtu ambaye hatakuwa na chembe ya uongozi unaotoka madarakani.
Mgombea kutoka Afrika (Liberia) Musa Bility ameongeza kuwa Platini ataleta makundi na migawanyiko ndani ya shirikisho hilo.Akiongea na shirika la utangazaji la uingereza BBC, Bility amesema Platini sio mabadiliko ambayo wote wanayakusudia.
Platini ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or mara tatu ana nafasi kubwa ya kushinda urais wa FIFA mara baada ya kupata sapoti toka kwa mashirikisho manne ya mabala duniani.Mkurugenzi wa shirikisho la soka la Scotland ni mmoja ya wanaompa sapoti Platini kwa madai amefanya kazi nzuri sana kwa UEFA.
Blatter miaka 79 ameongoza shirikisho hilo la mpira wa miguu tangu 1998.Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwakani February 26, wagombea watatangazwa rasmi October 26 mwaka huu.
Nini kinamsukuma Platini agombee?? Platini raia wa ufaransa anasema kuna wakati katika maisha unahitaji kukumbatia fursa zako.Platini anasema lengo lake ni kufanya kazi bila kuchoka ili kurudisha hadhi ya chombo hicho mahsusi ulimwenguni.
Anaendelea kuongea kwamba kupitia UEFA, ameweza kuyaunganisha mataifa madogo na makubwa kwa kutoa fursa sawa na kwamba atafanya hivyo pia katika ngazi ya dunia.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video