Sunday, July 19, 2015

Nadir Haroub 'Cannavaro'

Ukiwafuatilia makocha wengi Duniani, hupendelea kuwafundisha wachezaji kupiga penalti upande wa pembeni wa goli kuliko katikati.
Mpira ukipigwa pembeni ya goli una asilimia kubwa ya kuingia kwasababu ya kasi au Golikipa kuchelewa kufika, lakini katikati ni kama kuchezea shilingi chooni.
Kwa vile wachezaji wengine wana kiburi kutokana na uzoefu wao pamoja na utaalam, haamua kuleta vionjo katika upigaji wa penalti ingawa utundu huu unaweza kumfanya Shujaa au ziro kabisa.
Moja ya wanasoka wenye kiburi cha kupiga penalti za vionjo ni kiungo wa zamani wa Juventus, Andrea Pirlo ambaye hupendelea kupiga penalti aina ya panenka.
Aina hii ya penalti hupigwa katikati ya goli na kipa huhama upande wa kulia au kushoto, huku mpira ukipita katikati kwa juu. Panenka ni penalti ambayo inakuweka katikati ya ushujaa na u-ziro.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' aliwahi kupiga panenka dhidi ya Al Ahly ya Misiri katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika iliyopigwa mjini Alexandria, Misri, Yanga wakitolewa kwa matuta.
Cannavaro alionekana shujaa, alishangiliwa mno, lakini jana amejaribu kupiga panenka dhidi ya Gor Mahia na kuchemsha.
Makocha wanasemaje kuhusu Panenka?
"Penati ya namna ile wanaita Panenka ambayo unaweza kuwa shujaa au ziro, ukifunga wewe ni shujaa, ukikosa watu wanakuona wewe ziro. Nadir Haroub 'Cannavaro'  anatakiwa kubeba lawama, timu imepata penalti dakika za mwisho na inatakiwa kusawazisha kwenye mechi ya kwanza  na muhimu ya kombe la Kagame, yeye akaamua kupiga penalti ya Panenka.  Angefunga angeonekana shujaa. Ukipiga panenka inatakiwa golikipa ahame kutoka kulia kwenda kushoto, lakini kipa wa Gor Mahia kwa bahati mbaya hakuhama, Nadri Haroub anatakiwa kukubali lawama". Amesema mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele.
Makocha hufundisha kupiga penalti ya Panenka?

"Hakuna mwalimu yeyote anayeweza kuridhia au kumfundisha mchezaji kupiga penalti ya namna ile, walimu wote Duniani nikiwemo mimi nafundisha kupiga penalti pembeni, ndiko kuna asilimia nyingi za kufunga kutokana na kasi ya mpira au golikipa kuchelewa kufika. Penalti za katikati ya goli ni uwezekano tu, ni sawa na kuchezea shilingi chooni". Amefafanua Ally Mayay.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video