UWANJA wa Taifa jijini Dar es salaam jana ulilipuka kwa
Shangwe nyingi baada ya mshambuliaji wa
Yanga, Donald Ngoma kufunga goli la kuongoza mapema dakika ya nne, Yanga ikifa
2-1 dhidi ya Gor Mahia katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Kagame.
Mashabiki waliovalia jezi za rangi ya kijani na njano
walimtukuza Ngoma ambaye amekuwa mkali wa kufunga tangu atue Jangwani siku za
karibuni kutokea FC Platinum ya Zimbabwe.
Lakini furaha hiyo ilizimika baada ya Ngoma kupewa kadi
nyekundu kipindi hicho hicho cha kwanza baada ya kumfanyia 'uhuni' mchezaji wa Gor Mahia.
Hivi kadi nyekundu aliyopata Ngoma alistahili akiwa ni mchezaji
wa kulipwa?
"Hapana shaka kiwango cha Donald Ngoma kwa mechi ambazo
nimemuona, ni mshambuliaji ambaye anaweza kutegemewa kutokana na urefu wake,
uwezo wa kukaa na mpira, ana sifa za kufunga kwa kuibia na hata kwa kutumia
nguvu kutokana na umbile.".
"Bahati mbaya sana
hana 'Proffesional Altitude' ambayo ni kuwa makini, unajua unapokuwa
mchezaji mahiri na bora, unatakiwa kuwa makini na watu wanaokukaba na kuweza
kuzuia hasira. Kwa kadi nyekundu aliyopewa
(Ngoma) inaonekana ni mtu ambaye matukio yake yanaweza kuigharimu timu. Kadi ya
kwanza ya njano haikustahili kwa Proffesional Player kwasababu beki alikwenda
kuchukua mpira akamvuta mkono, lakini kadi ya pili mchezaji akawa kama
amemkanyaga akamvuta mkono. Kama mchezaji Proffesional anatakiwa kujiupusha na
matukio hayo, analipwa fedha nyingi, tena ametoka mbali huko Zimbabwe".
Amesema mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars ambaye kwasasa ni kocha na
mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay Tembele.a
0 comments:
Post a Comment