Waziri mkuu wa zamani wa iliyokuwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Kenya Raila Omolo Odinga (katikati) aipunga mkono kwa mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia pambano la Yanga dhidi ya Gor Mahia (kushoto) Mwenyekiti wa CECAFA Leodigar Tenga (kulia) katibu mkuu wa CECAFA Nicolas Musonye
Mgeni rasmi kwenye pambano la ufunguzi wa michuano ya Kagame Cup kati Yanga SC (Tanzania) dhidi ya Gor Mahia (Kenya) hakuwa Mh. John Pombe Magufuli kama TFF na CECAFA walivyotangaza siku chache kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi na badala yake alikuwa ni Wairi mkuu wa zamani wa iliyokuwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Kenya Mh. Raila Odinga.
Awali TFF ilitangaza kuwa Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli ambaye amechaguliwa na chama chake cha CCM kugombea kwenye kinyang’anyiro cha urais mwezi Oktoba mwaka huu ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya Ufunguzi, lakini pia katibu mkuu wa CECAFA Nicolas Musonye alithibitisha kwamba Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi kwenye mechi hiyo.

Raila Odinga (katikati) akiwa na mwenyekiti wa CECAFA Leodigar Tenga (kushoto) pamoja na Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) wakati nyimbo za taifa la Kenya na Tanzania zikiimbwa
Lakini mambo yalikuwa tofauti na matarajio ya wengi pale alipoonekana Laila Odinga akikagua timu na hapo ndipo watu wakagundua wamepigwa ‘changa la macho’ kwani siku zote anaekagua timu ndiye mgeni rasmi.
Ondinga alikuwa ameongozana na maafisa wa TFF na CECAFA akiwepo mwenyekiti wa baraza hilo Leodigar Tenga, katibu wake mkuu Nicolas Musonye pamoja na Rais wa TFF Jamal Malinzi.
Odinga aliwania urais wa Kenya mwaka 2007 kupitia chama cha upinzani cha Orange Democratic Movement maarufu kama ODM na kuleta upinzani mkubwa kwenye chama tawala cha Kenya. Machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi nchini humo kutokana na wananchi kupinga matokeo kwamba Ondinga ameshindwa uchaguzi, yalisababishwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, mwaka 2008 Odinga akawa Waziri mkuu wa Kenya.
Kwenye uchaguzi wa mwaka 2013, Odinga alishika nafasi ya pili kwenye kinyang’anyiro cha urais kwa kupata asilimia 43.28 za kura zote zilizopigwa wakati Uhuru Kenyatta alipoibuka kidedea.
Taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zinasema kwamba, jana Magufuli alikuwa jijini Mwanza na TFF walikuwa wakitambua hilo mapema lakini walishindwa kutoa taarifa kuwa Magufuli hatokuwepo kwenye uwanja wa taifa kama mgeni rasmi kushuhudia mtanange kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia ambapo Gor Mahia waliibuka na ushindi wa goli 2-1.
0 comments:
Post a Comment