Sunday, July 19, 2015

Mlinzi na kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele (wa pili kushoto) akitazama mechi ya Yanga dhidi ya Gor Mahia jana uwanja wa Taifa.
MOJA ya stori kubwa hapa mjini ni Mabingwa wa Tanzania bara, Young Africans kuchapwa  magoli 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya ufunguzi ya kombe la Kagame iliyopigwa jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Mashabiki wengi wa Yanga wameonekana kutokuwa na hofu hasa wakirudisha kumbukumbu zao nyuma ambapo walianza kwa kipigo,  lakini wakamaliza mashujaa kwa kutwaa ubingwa.
Takwimu haziongopi na kuna wakati zinajirudia, ingawa katika mpira huu wa kisayansi zinaweza kubaki kwenye makaratasi tu.
Mwaka 1993,  Wenyeji wa Kombe la Kagame wakiwa Uganda, mechi ya kwanza Yanga ilifumuliwa 3-1 na wenyeji SC Villa 'Jogoo', lakini walipokutana fainali Wanajangwani wakatoa risasi 2 - 1 na ndoo ikatua Jangwani.
Rekodi inayofanana na hiyo ikajirudia tena mwaka 1999, Wenyeji wa Kagame wakiwa wale wale Uganda.  Kipute cha kwanza Yanga ilifungwa na Rayon Sports ya Rwanda mabao 3 - 0, ikaingia fainali na SC Villa na kushinda kwa penati, shujaa akiwa ni Peter Manyika Sr.
Moja ya wachezaji waliokuwepo katika kikosi cha Yanga 1999 ni Ally Mayay Tembele ambaye amefanya mahojiano maalum na mtandao huu na kutoa  simulizi hii ya kusisimua.

Swali: Mwaka 1999 Yanga ilianza kwa kufungwa kombe la Kagame lililofanyika nchini Uganda na wewe ukionesshwa kadi nyekundu kama ilivyotokea kwa Donaldo Ngoma jana uwanja wa Taifa, lakini mkachukua ubingwa, tueleze mazingira ya kadi nyekundu uliyopata......

Ally Mayay: Hii ilikuwa mechi yangu ya kwanza ya kimataifa kuichezea Yanga, mpira ukawa unaingia golini, nikauzuia kwa mkono, nikapewa kadi nyekundu ya moja kwa moja pamoja na penalti, kiukweli walifunga wale Rayon Sports, ilikuwa mechi ya ufunguzi.

Swali: Said Mwamba Kizota alikuwa anacheza namba tisa na baada ya wewe kuoneshwa kadi nyekundu akarudi kucheza mkoba (mlinzi wa kati), hebu tukumbushe tukio hilo....

Ally Mayay:  Kweli Said Mwamba alikuwa namba 9, baada ya mimi kupewa kadi nyekundu ikabidi arudi kucheza nafasi ya beki wa kati . Baada ya mechi ile, mechi zote zilizofuata tulishinda. Tukaingia fainali na SC Villa, tukatoka droo ya moja moja ndani ya dakika 120 pale Nakivubo, tukaenda kupiga penalti,  tukashinda na mimi ndiye nilikwenda kupiga penalti ya mwisho ya kuchukua ubingwa .

Swali: Viongozi na makocha waliwaambia nini baada ya kufungwa mechi ya kwanza na kadi nyekundu juu?

Ally Mayay: Baada ya kupewa kadi nyekundu mechi ya kwanza tulikumbushwa na mwalimu Shungu pamoja na akina Said Mwamba Kizota kwamba  1993 walianza kwa kufungwa goli 3, lakini walikwenda mpaka wakachukua ubingwa.
Nasisi tukataka kuonyesha historia waliyoonesha mwaka 1993, walitupa moyo kwamba  1993 nao walipewa kadi nyekundu,  wakachukua ubingwa. Tukasema kadi nyekundu isituvunje moyo, mechi zilizofuata tulicheza vizuri, mimi nilikosa mechi iliyofuata tu, lakini nyingine zote mwalimu aliendelea kunipanga.

Swali: Mechi ya fainali dhidi ya Sports Club Villa, Said Mwamba Kizota alipewa kadi nyekundu, ilikuwaje mkapambana mpaka mwisho mkiwa pungufu?

Ally Mayay: Mechi ya fainali nakumbuka alipewa kadi nyekundu Said Nassor Mwamba Kizoto, tukacheza pungufu, lakini tulikuwa pungufu kwa dakika chache, tulifanikiwa kuwabana Villa mpaka dakika 120 na tukachukua ubingwa kwa Penalti.
Swali: Unaionaje nafasi ya  Yanga kutwaa ubingwa mwaka huu?

Ally Mayay: Nafasi bado ipo kwa Yanga, lakini mechi ya KMKM na Telecom ya Djbout sio ya kudharau. Bado Yanga wanaweza kufanya vizuri kama wataambiwa kwamba huko nyuma waliwahi kuanza kwa kupoteza na wakachukua ubingwa.

Kumbukumbu nyingine zinaonesha kwamba 2011, Tanzania wakiwa wenyeji wa kombe la Kagame, Yanga walitoka sare ya 2-2, fainali wakaingia na Simba na kuwafunga goli 1 - 0, bao la Kenneth Asamoah aliyemalizia krosi ya Kigi Makassy.
Mwaka 2012 Tanzania wakiwa wenyeji kwa mwaka wa pili mfululizo, mechi ya kwanza Yanga ikapigwa 2 - 0 na Atletico ya Burundi, fainali wakaingia  na Azam FC na kuwachapa mabao 2 - 0. Magoli ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi.

Mwaka huu wameanza kwa kichapo, swali ni je, Historia inaweza kujirudia?

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video