Higuain amefunga goli pekee lililoipeleka Argentina kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America inayozidi kushika kasi huko Chile. Goli la Argentina limefungwa mapema kipindi cha kwanza dakika ya 11, goli hilo liliipa Argentna ushindi wa goli 1-0 mbele ya Jamaica ‘Reggae boys’ ambao hawajashinda mchezo wowote kwenye kundi B.
Ushindi huo unaifanya Argentina kumaliza ikiwa kinara wa kundi B na huenda ikakutana na Ecuador, Peru au Venezuela kwenye mtanange wa robo fainali utakaopigwa siku ya Ijumaa.

Jose Gimenez alianza kuifungia Uruguay goli la kuongoza dakika ya 29 ya mchezo lakini Lucas Barrios aliisawazishia Paraguay goli hilo japo sare hiyo haijawasaidia Paraguay kusonga mbele kwenye mashindano hayo makubwa kwa bara la Amerika ya Kusini.
0 comments:
Post a Comment