Kocha Msaidizi wa Yanga,Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania kwa muda akisaidiwa na Selemani Matola.
Mkwasa ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya Yanga anachukua nafasi ya Mart Nooij aliyetimuliwa pamoja na benchi lake lote la ufundi baada ya Taifa stars kuchapwa goli 3 - 0 dhidi ya Uganda "The cranes".
Mara moja Mkwasa na Matola wataipokea timu hiyo kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Waganda hao.
0 comments:
Post a Comment