Tuesday, May 5, 2015

UONGOZI wa Yanga umetangaza kuachana na tabia ya kuzishangilia timu za nje pale timu za Tanzania zinapoiwakalisha nchi katika michuano ya kimataifa.
Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya Yanga kuwasili nchini kutokea Tunisia ilikotolewa na Etoile du Sahel kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 ambapo ilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa na kufungwa 1-0 huko Tunisia.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro leo amekutana na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Makutano ya Twiga na Jangwani, Kariakoo Dar es salaam na kufafanua mambo mbalimbali kuhusu safari yao ya tunisia.
"Timu zikienda kwenye michuano ya kimataifa basi tupeane sapoti na michuano hiyo ikiisha turudi kwenye upinzani wetu kama kawaida.Tusipeleke upinzani wetu kwenye mashindano ya kimataifa tutakosa vitu muhimu ambavyo vinaleta tija kwa taifa". Amesema Muro na kuongeza: "Sisi Yanga tutabadilika na tunaomba vilabu vingine vibadilike, maana hata wenzetu kule Tunisia walitucheka kwamba wao walipata mashabiki wengi walivyokuja huku lakini sisi kule hatukupata hata mmoja. Hivyo sisi tutaanza kwa kudilika na wengine wafuatie".
Pia Muro amesema kuhusu habari za usajili zinazoripotiwa si za kweli kwasababu uongozi bado haujapata mapendekezo ya kocha mkuu, Hans van der Pluijm. 
"Kuhusu usajili zinaandikwa habari nyingi kuhusu usajili wa Yanga. Sisi kama Yanga bado hatujapokea taarifa yoyote kutoka kwa mwalimu kama anamuhitaji mchezaji yoyote. Sasa hivi waandishi tunaomba mtusaidie kudumisha mshikamano wetu kama Yanga." Amesema Muro.
Aidha, Muro amefafanua uzushi kwamba Yanga wamepanga matokeo kuelekea mechi mbili zilizobaki dhidi ya Azam fc (kesho) na Ndanda fc mei 9 mwaka huu baada ya kufanikiwa kubeba ubingwa.
"Sisi kama timu tumejiandaa kama timu ya kawaida, kuna habari ilitolewa kwamba Yanga imepanga matokeo kwa mechi mbili zilizobaki. Sio kweli kabisa sisi kama Yanga tutacheza kama kawaida, kuchukua ubingwa kabla ya mechi mbili sio sababu ya sisi kupanga matokeo". Amefafanua Muro.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video