Monday, May 4, 2015

Arsene Wenger amemjibu Thierry Henry baada ya kusema kuwa Olivier Giroud pekee hawezi kuipa ubingwa Arsenal.
Kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Hull City, Wenger amemtetea Giroud ambaye mpaka sasa ana magoli 18 katika michuano yote na kusema kuwa mshambuliji huyo raia wa Ufaransa ana sifa zote ana anastshili kuwepo pale.
Henry ambaye kwa sasa ni mchambuzi katika kituo cha runinga cha Sky Sports, hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa“Arsenal wanahitaji mshambuliaji wa kiwango cha juu kabisa na chenye ubora ili kuweza kushinda taji la ligi kuu kwa mara nyingine tena tangu msimu wa 2003/04”.
“Naweza kukubaliana na maoni yake, lakini kauli yake juu ya Giroud sio sawa kabisa,"Wenger alisema.
Henry alisema kuwa Giroud anakosa vitu fulani hivi ambavyo Arsenal wanavihitaji.
"Hasa kwa sababu vitu kama hivyo pia vilisemwa kwa Nicolas Anelka, Thierry Henry mwenyewe na hata Robin van Persie ambao wamekuwa ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa duniani."
Wenger aliongeza kuwa Henry anashawishika kuongea vitu vyenye kuvuta hisia za wengi zaidi kwa sabau ya kazi yake hiyo mpya aliyopewa pale Sky Sports.
“Nadhani hayuko sahihi. Analipwa kwa hilo ndio maana,"Wenger alisisitiza.
Olivier Giroud - Premier League 2014/15
 Minutes played     Goals             Assists
      1506                    14                      3     
"Wote tunafahamu mifumo ya vyombo vya habari vya kisasa vinavyoendeshwa, hasa TV. Wanakufanya utoe kauli za utata utata kwa sababu wanakulipa pesa nyingi sana.
“Unaitathmini timu yako kwa mafanikio yake ulimwenguni. Ninachokifahamu ni kwamba Giroud anajituma sana kwa ajili ya timu na ana fikra chanya siku zote na kama timu inafanya vizuri basi ujue ni kwa ajili yake, na pia anafunga zaidi ya magoli 20, basi ametimiza wajibu wake.”

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video