Monday, May 4, 2015

Mwaka jana mwishoni, Mtangazaji wa redio moja huko nchini Marekani Kelly Mac alimuuliza mwanamasumbwi mwenye rekodi ya kipekee duniani Floyd Mayweather kwamba ana pesa nyingi, kwa nini asiisaidie Afrika?.
Hapa anaeleza......
Hapo awali mwanamasumbwi huyo alijinasibu kwamba ana roho nzuri, lakini haoni kama kuna sababu ya yeye kutoa misaada barani Afrika. “[watu] wanasema ‘kweli una pesa nyingi, kwa nini hutoi misaada barani Afrika?’” Mayweather anasema. “swali zuri, ni kipi hasa Afrika imetufanyia sisi? Ni kipi hasa Afrika wamefanya kwa watoto wangu na familia yangu kwa ujumla? Lazima vitu vifanyike kwa pande zote mbili.”
Baadaye akasema kutoa kulikopitiliza kunaweza sababisha ufilisike.
“Kila mtu anasema kuhusu, kutoa, kutoa, kutoa. Hilo ni tatizo.Watu wanafanya hivyo lakini mwisho wa siku wanafilisika kabisa, halafu utasikia watu wanasema badala angekuwa anatunza hela zake na kufanyia mambo mengine yeye alikuwa anagawa tu, kwa nini asingekuwa anahifadhi sasa?’” Mayweather alienda mbali zaidi na kusema, hela anazopata hapaswi kupangiwa cha kufanya na mtu yeyote yule, akiamua kutumia yeye na familia yake ni maamuzi yake mwenyewe.
“Sikujiingiza kwenye mchezo wa ngumi na kusema‘kwamba naenda sasa kupigana na kutengeneza mamilioni ya fedha ili nigawe tu kwa watu.’ Kama natumia hela vibaya, ni mimi mwenyewe. Nafanya nitakacho na fedha zangu.
Unasikia watu wanasema kwamba, ‘angechangia hapa, angechangia pale.’ Hapana, Ninatakiwa kuchangia kwa Floyd Mayweather, pia kuchangia kwa familia ya Floyd Mayweather. kwa sababu ndivyo vinavyonihusu.”

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video