WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefikisha pointi 44 katika
nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 25, pointi moja nyuma ya Azam fc waliopo
nafasi ya pili kufuatia kushuka dimbani mara 24.
Magoli ya Ibrahim Hajib dakika ya 48 na Ramadhan Singano
dakika ya 64 yalitosha kuwapa Simba dhidi ya Azam fc katika mechi ya ligi kuu
iliyopigwa jana uwanja wa Taifa. Goli la Azam lilifungwa na kiungo Mudathir
Yahya dakika ya 58.
Ili Simba wachukue nafasi ya pili wanahitaji kushinda mechi
ya mei 9 dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Taifa, halafu Azam wafungwe na Yanga kesho
kutwa na kutoa sare mechi ya mwisho
dhidi ya Mgambo JKT.
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic baada ya kufanikiwa
kuzifunga timu mbili za juu msimu huu, Yanga na Azam, amesema sasa swali la
timu gani bora nchini limeshajibiwa.
“Niliiandaa vizuri timu yangu, Azam fc ni mabingwa na bado
nawaona ni mabingwa, ni timu ngumu, nina furaha sana kwasababu nilikuwa na
msongo wa mawazo, sio mimi tu, kila mtu ndani ya timu’. Amesema Kopunovic na
kuongeza: “Nina furaha sana, najivunia sana kuwa timu yangu ndio bora nchini
Tanzania, tulimfunga Yanga, tumemfunga Azam, nadhani hakuna swali tena ni timu
gani bora Tanzania”.


0 comments:
Post a Comment