Monday, May 4, 2015

JOSE Mourinho amekiri kuwa alihatarisha heshima yake kwa kukubali kurudi Chelsea na ilionekana kama amemuogopa mpinzani wake mkubwa Pep Guardiola wakati huo akiwa Real Madrid.
Upinzani wa Mourinho na Guardiola ulishamiri zaidi pale walipotawala soka la Hispania, Mourinho akiwa na Real Madrid na Guardiola akiwa Barcelona.
Mourinho ambaye anafurahia kufanya kazi dhidi ya wapinzani wake amesema yawezekana angeenda kwenye ligi rahisi ambapo hata mtunza vifaa wa timu anaweza kuwa bingwa.
Kauli hii inampiga dongo Guardiola ambaye alikwenda Bundesliga kuifundisha Bayern Munich na msimu huu ameshinda kombe.
"Mimi sio mtu bora zaidi wa kuchagua mataifa na klabu. Labda ningechagua klabu nyingine na taifa lingine ambalo kushinda kombe ni rahisi sana".
"Nilichagua klabu ambayo nilikuwa na furaha kabla na taifa ambalo nilikuwa na furaha kabla. Nilijipalia mkaa. Nina furaha sana, sana ya kushinda kombe lingine tena la ligi kuu miaka 10 badaye baada ya kushinda la kwanza"
"Nimekuwa bingwa kila klabu niliyofundisha. Nimefundisha Inter, Real Madrid na Chelsea. Kila kombe lina maana kubwa kwangu, kushinda kombe Hispania kwa pointi 100 dhidi ya klabu bora ya Barcelona yalikuwa mafanikio makubwa mno.
"Labda siku za usoni nitakuwa bora na kuchagua klabu na taifa lingine ambalo kila mtu ni bingwa. Labda nitakwenda nchi ambayo hata mtunza vifaa anaweza kuwa kocha na kushinda kombe."
Ninafurahia magumu ninayokumbana nayo. Nadhani niko eneo sahihi. Nipo hapa mpaka mmiliki wa timu Roman Abramovich atakaponiambia niondoke".

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video