KLABU ya Yanga imewanasa wachezaji watatu hatari raia wa Ghana ambao imeelezwa ni chaguo la Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, akiamini wanaweza kumsaidia kufanikisha mipango yake ya kuifanya timu hiyo kuwa tishio barani Afrika.
Kati ya wachezaji hao wanaochezea klabu ya Modeama FC ya Ghana, kwa mujibu wa gazeti la BINGWA, limenasa jina kamili la kiungo mkabaji ambaye ni Victor Ayirey, wakati mwingine ni beki wa kati aliyetajwa kwa jina moja la Dakwah, huku mwingine jina lake likiwa bado halijajulikana.
Chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Yanga kimesema kuwa, wachezaji hao wanatarajia kutua nchini Juni 6, mwaka huu, wakiongozana na Pluijm aliyepo mapumzikoni Ghana.
Alisema kuwa mara watakapowasili wachezaji hao wataungana na wenzao kwa ajili ya mazoezi yatakayoanza siku inayofuata, ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame.
0 comments:
Post a Comment