Uongozi wa Free State Stars inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika kusini umekubali ombi la Mrisho Ngassa kupewa jezi namba 17 ambayo
amekuwa akiitumia.
Blog ya michezo ya Salehjembe amemkariri meneja wa Free State Stars, Motuba Mokoena akisema
Ngassa ameomba kupewa jezi namba 17 aliyoitumia
wakati anacheza Kagera Sugar, Yanga na
Simba, na mpaka sasa anaitumia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
“Ngassa ameomba tumpe jezi na kumi na saba. Tumeona hilo
linawezekana na tutalifanyia kazi.
“Naweza kusema ni uhakika tutampa jezi hiyo na kazi ya
kuwakabidhi jezi mpya wachezaji wote itafanyika rasmi leo,” Meneja huyo ameiambia Salehjembe.
Tayari Ngassa yuko Afrika Kusini ambako amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa
miaka minne.
Baada ya kukabidhiwa jezi, leo, Ngassa ataondoka kwenda
kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya
Cosafa inayofanyika nchini humo.
0 comments:
Post a Comment