Jemedari (kulia) ameitosa Azam fc
MENEJA wa Azam fc, Jemedari Said Kazumari amemaliza mkataba wake na
klabu hiyo yenye masikani yake maeneo ya Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es
salaam na kuamua kuachana nayo na sasa amepata kazi mpya ndani ya Shirikisho la soka nchini, TFF.
Jemedari, mchezaji wa zamani wa Kariakoo ya Lindi ameajiriwa
na TFF kuwa Afisa Maendeleo (Development Officer) na anakuwa msaidizi namba
moja wa mkurugenzi wa ufundi wa TFF
(Technical Director), Salum Madadi.
Cheo hicho alichoajiriwa Jemederi kilikuwa kinashikiliwa na
Dr. Jonas Tiboroa kabla ya kuajiriwa Yanga katika nafasi ya katibu mkuu.
Miaka ya nyuma, Madadi ndiye aliyemuibua Jemedari kutoka ligi
daraja la tatu na kuwa mchezaji wa Kariakoo ya Lindi ambayo ilikuwa inafundishwa na Madadi wakati huo na sasa wanakutana tena katika ngazi ya uongozi.
Siku za karibuni Jemedari hakuwa na mahusiano mazuri na
Afisa mtendaji mkuu wa Azam fc, Saady Kawemba na siku walipotoka sare ya 1-1
dhidi ya Mbeya City uwanja wa Azam Complex mwaja huu, waliripotiwa kukunjana mashati hadharani, lakini baadaye
wote walikanusha kuwa hawana ugomvi wakidai hiyo ni migongano ya kawaida
kiutendaji.
0 comments:
Post a Comment