Kocha wa Crystal Palace Alan Pardew amemsifu Jose Mourinho baada ya kushinda pambano dhidi ya timu yake katika uwanja wa Stamford bridge na kutangaza rasmi ubingwa kwa msimu wa 2014/05.
Eden Hazard alifunga goli pekee ambalo hapo awali mkwaju wake wa penati uliokolewa na Julian Speroni kabla ta kuunganisha tena kwa kichwa na kuipa ubingwa timu yake.
Pardew pia amezungumzia suala la mfumo wa Mourinho wa kupaki basi na kusema kuwa hicho ndicho kinachomfanya Mourinho ashinde makombe mengi zaidi.
"Ukiangalia kwa umakini wamepoteza michezo miwili tu msimu mzima. Sidhani kama kuna mtu anayeweza kukosoa jinsi walivyocheza katika raundi ya kwanza ya ligi," Pardew aliiambia Sky Sports.
"Wakati mwingine timu inaweza kupotea sasa kinachotakiwa ni kutumia mbinu mbadala ili kuweza kushinda tu, na hicho ndicho walichokifanya katika raundi ya pili. Ndiyo maana utaona kuwa kijana [Mourinho] anapata pesa nyingi kwa kushinda vikombe.
"Ina nafasi kubwa sana ya kuongoza tena ligi msimu ujao. Nina uhakika kabisa Jose ataongeza wachezaji kadhaa ili kumarisha zaidi kikosi chake.
"Ni wagumu sana kama ukiwaacha waanze kukutangulia, hasa katika uwanja wao."
0 comments:
Post a Comment