Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm (kulia) akiwa na msaidizi wake, Mkwasa (wa pili kulia)
KOCHA msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameanika udhaifu walioukuta katika kikosi cha Yanga walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa klabu hiyo yeye na bosi wake Hans van der Pluijm mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na mtandao huu, Mkwasa amesema: "Kila binadamu ana uzuri na mapungufu yake, tunaheshimu sana kazi kubwa waliyofanya Maximo (Marcio) na Neiva (Leonardo), lakini kama nilivyosema kila binadamu ana mapungufu yake". Amesema Mkwasa na kuongeza: "Tulipokuja na Hans (Van der Pluijm) tulikuta Yanga imekosa vitu vikubwa viwili, utimamu wa mwili na nidhamu".
"Wachezaji hawakuwa na uwezo wa kumudu muda, hawakuwa na nguvu, hawakuwa na nidhamu. Sisi tulichokifanya ni kuwaongezea utimamu wa mwili na nidhamu ya mchezo. Pia tukawafundisha kucheza kwa kasi, kushambulia na kumiliki mpira".
"Mwanzoni uliona timu inafunguka japokuwa ushindi ulikuwa wa magoli machache, lakini kadiri siku zinavyoenda unaona timu inashinda magoli mengi".


0 comments:
Post a Comment