Saturday, May 9, 2015

Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United, ndiyo kimeishusha Ruvu Shooting hadi daraja la kwanza.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amekubali kipigo lakini akasisitiza: “Ilikuwa utafikiri hawako Tanzania.”
“Walikuja vijana na mapanga hadi hotelini kwetu, walitutishia. Ikafikia tukashitaki kwa mabosi wa polisi lakini hakuna aliyetusaidia.
“Nikalazimika kuwasiliana na kuwasiliana na makao makuu ya Polisi kupitia Chagonja, ndiyo tukapata msaada.
“Lakini tulipoingia vyumbani, mambo yalikuwa mazuri. Tulipotoka kwenda kupasha mwili, kosa kubwa.
“Tumerudi vyumbani kuna harufu kali ya dawa iliyopuliziwa kwa ajili ya kupunguza nguvu ya mwili. Hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaumiza vijana. Kamisaa ameona, nimemuita na harufu kaivuta pia, waandishi wameona.
“Achana na hivyo, tulipambana sana uwanjani lakini mwamuzi alikuwa kama ni mtu aliyepewa maagizo kwamba sisi lazima tufungwe,” alisema Masau ambaye timu yake itacheza daraja la kwanza msimu ujao.
Chanzo:Salehe Jembe

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video