Monday, May 11, 2015

Nguli wa Brazil Ronaldo amesema kwamba kwa sasa hakuna wachezaji nyota wa katika ulimwengu wa soka licha ya uwepo wa Lionel Messi,Neymar na Cristiano Ronaldo.
Ronaldo na Messi ndio wachezaji wawili pekee ambao wameshinda tuzo ya mchezaji bora wa duniani ndani ya miaka 7, huku Neymar naye akionekana kuja kwa kasi kuiwania tuzo hiyo.
Hata hivyo, Ronaldo - ambaye amezichezea klabu hizo kubwa mbili za nchini Uhispania -anaamini kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya wachezaji hawa watatu na wengine waliobaki katika ulimwengu wa soka.
"Kama alivyosema Zinedine, nadhani Messi ni wa ajabu, Ronaldo anshangaza na Neymar ni wa ajabu pia lakini nadhani ulimwengu wa mpira wa miguu unawakosa baadhi ya nyota muhimu," alinukuliwa alivyokuwa akiongea na Marca.
Ronaldo '38' kwa upande wake hataki kukubaliana na Zidane ambaye hapo nyuma wote wamewahi kuichezea Madrid.
"Ni rafiki yangu yule na tunaongea vitu vingi sana kuhusu mpira hata leo. Kwa sasa yeye ni kocha, lakini hilo ni suala moja ambalo sikubaliani naye hata kidogo.
"Msukumo ni ule ule, ila sio ule ambao unaupata ukiwa uwanjani."
Ronaldo amesema kuwa angeweza kurudi uwanjani akiwa kama mshambuliaji wa Fort Lauderdale, klabu ambayo ana hisa pale.
"Ni kitu ambacho nataka sana kukifanya, lakini sijui kama nitaweza. Nikicheza nahisi maumivu kwenye misuli. Niliacha kucheza kwa sababu ya maumivu ya nyonga. Yalikuwa ni maumivu mabaya sana ambayo sikuwahi kuwa nayo hapo awali, hii ilinifanya kupoteza kasi yangu uwanjani."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video