Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KIUNGO mshambuliaji wa Mgambo Shooting Stars, Fully Maganga, ameweka wazi kwamba timu yao ilikuwa na lengo la kumaliza ndani ya nafasi tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu uliomalizika jana.
Katika mahojiano na mtandao huu jijini hapa leo, Maganga amesema wameshindwa kutimiza malengo yao msimu uliomalizika kutokana na sababu mbalimbali.
"Kuna matatizo mengi kwenye ligi. Ratiba kupanguliwa mara kwa mara na mengine mengi. Tulipanga kumaliza ndani ya nafasi tatu za juu msimu huu lakini tumenusirika kushuka.
"Tunamshukuru Mungu kwa kutoporomoka daraja, tutajipanga kwa ajili ya msimu ujao," amesema Maganga.
Mgambo Shooting imemaliza nafasi ya 12 VPL ikiwa na pointi 29 sawa na Ruvu Shooting Stars walioporomoka daraja.

0 comments:
Post a Comment