NAHODHA msaidizi wa Simba, Jonas Gerard Mkude amesema haya
kuhusu klabu yake ya Simba kuhusu kutoshiriki michuano ya kimataifa kwa miaka
miaka mitatu:
“Simba ni timu yenye
vijana wengi wenye uchu wa mafanikio, timu kubwa kama Simba kutocheza michuano
ya kimataifa kwa miaka mitatu ni aibu, tumepambana sana, lakini mpira wakati
mwingine unakwenda na bahati. Tunashukuru tumepata matokeo mazuri dhidi ya Azam
fc, hii ni timu bora kila mtu anajua, tumecheza vizuri na kuwadhibiti.
Tunajipanga kuelekea mechi ya mwisho dhidi ya JKT Ruvu”.
Mkude alicheza kwa kiwango cha juu Simba ikishinda 2-1 dhidi
ya Azam fc jana na ameahidi kufanya vizuri mechi ya mwisho dhidi ya JKT Ruvu
mei 9 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment