MSHAMBULIAJI wa Azam fc, Didier Kavumbagu ametamka wazi kuwa
anahitaji mapumziko katika mechi mbili za ligi kuu zilizosalia kwani amechoka
sana kutokana na kutumika kwa muda mrefu.
Azam imebakiza mechi mbili kumaliza msimu huu ambapo kesho
itacheza na Yanga uwanja wa Taifa na mei 9 mwaka huu itachuana na Mgambo JKT
uwanja wa Azam Complex.
Kavumbagu kesho anatakiwa kukutana na klabu yake ya zamani
ambayo siku za karibuni imekuwa ikihusishwa kumrejesha katika dirisha la
usajili la majira ya kiangazi mwaka huu, hivyo kuomba kupumzishwa ni kuikacha
kiaina.
Kavumbagu ambaye alifunga goli moja katika sare ya 2-2 baina
ya Yanga na Azam fc desemba 28 mwaka jana.
Lakini uongozi wa Azam kupitia kwa meneja wa klabu hiyo, Jemedari Said Kazumari
umeshangazwa na taarifa za Kuvumbagu kusema nje ya utaratibu, ila bado
hawaamini kama ni kweli kwasababu wachezaji wote wameshaelekezwa namna ya
kuzungumza na wapi kwa kufikisha mahitaji yao.
“Sidhani kama amechoka kufikia hatua hiyo, na kama ni hivyo
angemwambia mwalimu, kama amesema nje ya utaratibu si sahihi, lakini ni kitu
ambacho sikiamini’, Amesema Jemedari na kusisitiza: “Tulishazungumza na
wachezaji jinsi ya kufikisha taarifa au kuzungumza mambo yanayowahusu wao na
timu, sidhani kama Didier (Kavumbagu) hakuelewa kiasi hicho kwasababu tuko naye
kwa mwaka, taratibu anazijua, kama amezungumza kwamba amechoka hawezi kucheza, anajua utaratibu na mipaka yake ya
kuzungumza na nani anazungumze naye”
0 comments:
Post a Comment