Fabregas (katikati) anaamini timu yake inaweza kuwa bora zaidi barani Ulaya
CESC Fabregas amefurahia mafanikio aliyopata Chelsea msimu huu na kuamini kuwa timu hiyo inaweza kuwa bora zaidi barani ulaya.
Baada ya kubeba ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu England,Fabregas amekitabiria makubwa kikosi cha Chelsea chini ya Jose Mourinho pamoja na nyota wake, Eden Hazard.
Kuhusu Hazard, Mhispania huyo amesema anaweza kufikia mafanikio ya Lionel Messi, huku akidai Jose Mourinho yuko juu zaidi ya Arsene Wenger na Pep Guardiola, makocha waliowahi kumfundisha.
"Anajua namna ya kuiendesha timu (Mourinho) na namna ya kupata ubora wako,' amesema Fabregas. "Hiki ndicho unachohitaji kutoka kwa meneja, kwa asilimia 100. "Anaweza kumshawishi mchezaji kila baada ya siku tatu-sio jambo rahisi kwasababu unacheza mechi 60 kwa msimu, niamini mimi"
"Kila mtu anadhani tuna kikosi kikubwa, lakini hatuna. Tumetumia wachezaji 22, wengine ni kutoka kikosi cha chini ya miaka 21, kwahiyo si jambo rahisi na anafanya kazi kubwa".

Mourinho (kulia) ni bora kuliko Wenger na Guardiola-kwa mujibu wa Fabregas
Kuhusu mchezaji bora wa mwaka wa PFA, Eden Hazard, Fabregas amemfananisha na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi.
"Kwa kweli anaweza kuwa kama wao (Messi),' amesema Fabregas: "Anaweza kuwa juu. Alikuwa na msimu wa ajabu, nataka arudie tena msimu ujao na awe bora zaidi. Ni mtu muhimu na kwa akili yangu ndiye aliyeifanya timu hii iwe bora kwa kiasi kikubwa".
0 comments:
Post a Comment