Tuesday, May 5, 2015

Na Richard Bakana, Dar es salaam
MLINDA mlango wa klabu ya Simba, Ivo Mapunda amekaribisha ofa mbalimbali kwa timu zitakazo hitaji huduma yake baada ya mkataba wake na wekundu hao wa Msimbazi kuelekea ukingoni huku viongozi wa timu wakiwa kimya kumueleza hatima yake.
 Mkataba wa Ivo, kipa wa zamani wa Prisons, Yanga, Saint George na Gor Mahia  unamalizika mei 20 mwaka huu kwa maana hiyo amebakiza siku 15 tu.
 Ivo Mapunda amesema kuwa anafurahia maisha ya Simba ambao ndio waajiri wake kwa sasa, lakini yupo tayari kufanya kazi sehemu yoyote kama watavutiwa na huduma yake.
“Mimi nafanya kazi vilevile hadi nitakapomaliza mkataba, watakapotaka kunipa mkataba,  mimi nipo tayari Kusaini sehemu nyingine. Hapa ni Nyumbani, Simba ni timu yangu na ninafurahia maisha yangu, bado sipo huru kwasababu Mkataba wangu bado haujaisha hadi Mei 20” Amesema Ivo Mapunda ambaye aliiongoza Simba  kuifunga Azam FC 2-1 uwanja wa Taifa mwishoni mwa juma lililopita. 
Ivo amesema  kuwa klabu yake bado ina uwezo wa kupata  nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya mchezo wa kupata ushindi juzi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video