Tuesday, May 5, 2015


Na George Mganga, Dar es salaam
Napenda kutoa pongezi kwa uongozi mzima wa klabu ya Yanga kwa hapo walipofikia katika msimu mzima wa ligi ambapo wamekuwa mabingwa wapya 2014/2015.
Licha ya ubingwa tumeona pia timu imeimarika na kufanya vyema katika hatua za awali za Kombe la shirikisho Africa japo imetolewa na Etoile du Sahel.
Na sitosita kutoa pongezi kwa uongozi mzima wa klabu hiyo kwa mikakati ambayo imekuwa ikionesha matokeo chanya haswa katika ligi kuu Vodacom ya msimu huu.
Ukiiangalia Yanga kama timu kwasasa bado utaona ile teamwork au ushirikiano baina ya wachezaji kiujumla wanaelewana vizuri pindi wanapokuwa mchezoni.
Si nafasi ya ulinzi, nafasi ya kati, viungo na hata mawinga na washambuliaji kiujumla katika kikosi chote mambo yapo vizuri na kama kuna pengo bado halijachipukia kwa hali ambayo inaweza kuleta udhaifu katika timu.
Kikubwa ninachoumba uongozi wa timu wawe na uvumilivu na kikosi bila kupepesa macho na hakina budi kuboreshwa kutokana na uimara ambao upo hivi sasa.
Ni wakati mzuri wa timu na uongozi kuangalia mapungufu yapi ambayo yapo katika timu katika kikosi cha sasa na kuyafanyia marekebisho kwaajili ya msimu ujao na mechi zijazo hapo mbeleni.
Labda katika mapendekezo yangu nafasi ya beki kuna uwezekano wa kuongeza namba 3 na halikadhalika pia inawezekana Mbuyu Twite akawa namba 6 na hapo sasa itakuwa anapanda mbele kidogo.
Suala la kuchukua ubingwa lisiwe la kubweteka sasa na kusahau yale yote ambayo yanakuja huku mbele kwa kudhania kutakuwa na mteremko na badala yake kunaliwa na milima.
Njia nzuri ya mafanikio huanza asubuhi pindi mtu unapoamka ukiwa na fikra chanya za kuleta maendeleo katika taifa lako pia malengo na ndoto za mafanikio huanza tangu utotoni binaadam akiwa mchanga.
Ni hatua nzuri kwa Yanga kuiona hapo ilipofikia katika michuano ya kimataifa na kukutana na timu kama Etoile du Sahel huku ikionesha kiwango kizuri kabisa licha ya kutolewa ni muda mzuri wa kukiendeleza kikosi kilichopo.
Mabadiliko ya kikosi kwasasa hayana mantiki kabisa katika timu hiyo kwani itachochea tena kurudisha nyuma maendeleo sawa sawa na kutafuta sindano ndani ya bahari jambo ambalo sio rahisi.
Unapobomoa kikosi na kukijenga upya tena inakuwa ni kazi mara mbili haswa kwa mwalimu na benchi zima la ufundi kuanza kuangalia tena nani aanze na nani aanzie benchi.
Pia ni wakati sahihi na mwafaka kuangalia ni wachezaji wapi hawana nafasi katika timu wapelekwe sehemu kwa mkopo au wauzwe kabisa maana tunajua wapo wale wanaokalia benchi tu na hawana nafasi katika kikosi hicho.
Jambo la Hans kuendelea kuinoa Yanga bado ni Mwalimu sahihi kabisa na ninampa asilimia 100% maana tangu arejee na kuchukua nafasi ya Maximo ameleta uhai kwa muda mchache na timu imekuwa komavu kimpira.
Haya masuala ya kubadili waalimu mara kwa mara hurudisha motisha na ari ya timu nyuma na badala yake kuleta hasara tu ya kutumia pesa nyingi kutafuta waalimu kila siku.
Ikumbukwe kuwa kikosi kipo katika nafasi ya kushiriki tena kwa mara nyingine michuano ya kimataifa na hii ina heshima kubwa zaidi kwa hiyo jambo la msingi ni kuona kikosi ambacho kipo hivi sasa kinaendelezwa.
Umakini juu ya haya ni silaha tosha ya maangamizi kwaajili ya matokeo mazuri katika timu na ndoto za kikosi kufika mbali zaidi na sio kuwa na uongozi wenye uroho wa madaraka bila ya kujali uwepo wao katika timu.
Siri nyingine ya timu kufanya vizuri ni klabu kufanya mechi nyingi za kitafiki ili kuwaweka wachezaji katika ari nzuri haswa kwa wakati huu ambapo wapo likizo.
Timu zetu hapa Tanzania mara nyingi zinlmekuwa hazilizingatii hili suala suala maana mara nyingi msimu wa ligi unapoisha wachezaji huwa wanakosa posho pamoja na mishahara jambo ambalo huwafanya wakimbilie kwenye ndondo.
Unapokuwa unawapa wawachezaji likizo ya muda mrefu haya ndiyo huwa yanatokea tofauti na unapotoa likizo ya muda mfupi ambapo wachezaji wanakuwa karibu zaidi na timu.
Ni vizuri zaidi tukiiga mambo hadi ambayo yanawafanya wachezaji kuwa katika morali na uwezo mzuri zaidi uwanjani kwa kuangalia wenzetu katika ligi za Ulaya kipi huwa wanafanya.
Nadhani Tanzania ipo siku itaheshimika kama nchi za Africa Magharibi japokuwa sio rahisi kufikia endapo tutazingatia haya.
Kama una chochote cha kuchangia juu hili nilichokiandika hapa mawasiliano yangu ni haya hapa.
0688665508

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video