Friedel ,
43, aliingia Uingereza mwaka 1997, kujiunga na majogoo wa jiji, klabu ya
Liverpool lakini pia amezichezea Blackburn, Aston Villa na Tottenham Hotspur anayoichezea
hivi sasa kama golikipa.
Kama Muamerica
huyo atacheza mechi yoyote ya Spurs kati ya mbili zilizobaki msimu huu basi
atakuwa ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia kuwahi kucheza
kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League)
Brad
Friedel ni moja kati ya makipa watano tu katika Ligi Kuu ya Uingereza kuwahi
kufunga goli. Wengine ni Paul Robinson, Peter Schmeichel, Asmir Begovic na Tim
Howard.
“Najivunia
sana kwa nilichovuna katika kazi yangu”
Alisema, “Siku nilipoanza safari yangu sikufikiri kama ingekuwa ndefu
hivi”
Friedel,
ambaye atatimiza miaka 44 mnamo tarehe 18 Mei, alisema atakumbuka ile hali ya
mazoea ya kila siku aliyokuwa nayo kwa wachezaji wenzake na wafanyakazi wa
klabu.
Aliongeza,
“Siku yangu ya kutimiza miaka 44 imefika (inakaribia) kwa hiyo nadhani ni muda
muafaka wa mimi kupumzika”
Friedel
anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi mfululizo katika Ligi
Kuu – mechi 310, kati ya Agosti 2004 na Novemba 2012 - pia ni moja ya makipa
watano tu waliofunga goli kwenye Ligi Kuu.
Alijiunga
na Spurs mwaka 2011 na kwa sasa tayari anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wao
mwenye umri mkubwa zaidi. Lakini
hajacheza mechi yoyote msimu huu, mechi yake ya mwisho kucheza ilikuwa ni
Novemba 2013.
Endapo
Friedel atacheza dhidi ya Hull City au Everton katika mechi mbili za Spurs
zilizobaki kwenye Ligi Kuu, hiyo itamfanya
ampite kipa wa zamani wa Manchester City, John Burridge ambaye ndiye
anashikilia rekodi ya kucheza mechi ya Ligi Kuu akiwa na umri mkubwa zaidi,
miaka 43 na siku 162.
“Nimekuwa
na wakati mzuri sana hapa na nimekutana na watu wengi wakubwa pia katika safari
yangu” aliongeza Friedel, ambaye ameichezea timu ya mpira wa miguu ya Marekani
(USA) mechi 82. “Hii ni klabu nzuri sana ya mpira wa miguu na najihisi
kuheshimika kuwa sehemu yake kwa miaka minne”
Friedel
amepanga kumalizia masomo yake ya ukocha ili apate leseni yake ya juu ya ukocha
(Pro-Coaching Licence) pia atakuwa
akifanya kazi katika vituo vya habari na lingine ni kuwa balozi wa klabu yake
ya Tottenham.
0 comments:
Post a Comment