Ligi kuu ya Hispania sasa itaweza kuendelea tena
wikiendi hii baada ya kusitishwa kwa wiki nzima
na Shirikisho la Mpira wa Miguu
la Hispania (Spanish Football Federation – RFEF) na mgomo wa wachezaji
kuisha.
Baada ya Mahakama Kuu ya Hispania kusema kuwa mgomo
wa wachezaji kuhusu haki za televisheni
si halali/si wa kisheria (unlawful), Shirikisho nalo lilibadilisha kauli yake
kwamba ‘msimu umeisha’
Barcelona inaweza kushinda taji la La Liga Jumapili hii, kabla mechi ya mwisho
haijachezwa, endapo itawafunga mabingwa, Atletico Madrid.
Mechi ya Kombe la Mfalme nayo itachezwa kama
ilivyopangwa, tarehe 30 Mei. Barca – ambao pia wamefikia fainali ya Ligi ya
Mabingwa barani Ulaya, watakayovaana na kibibi kizee cha Turin, Juventus –
watacheza na Athletic Club Bilbao kwenye Uwanja wa nyumbani, Camp Nou kwenye
fainali hiyo ya Kombe la Mfalme.
Mwandishi
habari za soka nchini Hispania, Andy West anaelezea mgogoro huu:
“Kimsingi, usitishwaji wa ligi ulikuwa ni matokeo ya vita ya madaraka
juu ya nani anaendesha mpira wa Hispania. Ni dhahiri kabisa, hiki ni kilele cha
mgogoro wa muda mrefu juu ya mgawanyo wa mapato ya televisheni ambayo yamekuwa
yakipimwa kwa kuwapendelea ‘wakubwa
wawili’ wa Barcelona na Real
Madrid.”
Shirikisho na umoja wa wachezaji (AFE) zimeridhika
na sheria mpya inayojumuisha majadiliano ya bei juu ya haki za televisheni kwa
mechi za ndani , inayoungwa mkono pia na
wasimamizi wa Ligi ya Mpira wa Kulipwa
nchini humo (National Professional Football League – LFP), inayoendesha ligi
mbili kubwa za kulipwa nchini humo.
Wachezaji waliounga mkono mgomo wanaamini mgawanyo
wa pesa kwenye mkataba mpya
uliopendekezwa na LFP na serikali ya Hispania hauwanufaishi wale wanaozichezea
klabu za chini/ ndogo.
Ijumaa iliyopita, Raisi wa LFP, Javier Tebas
alitangaza mipango ya kwenda mahakamani dhidi ya usitishwaji wa ligi, huku
akionya italeta hasara ya mapato hadi €
50 milioni (zaidi ya bilioni mia, shilingi za Tanzania) kwa mechi za mzunguko
mmoja.
Hii
Ndio Ratiba ya Mechi
Kali Zilizobaki Hispania.
Jumapili,
17 Mei: Atletico Madrid
v Barcelona
Espanyol
v Real Madrid
Jumamosi, 23 Mei:
Barcelona v Deportivo
Real Madrid v Getafe
Jumamosi, 30 Mei:
Fainali ya Kombe la Mfalme
Athletic Bilbao v
Barcelona
0 comments:
Post a Comment