
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
"Kampuni ya Bin Slum Tyres pia inadhamini timu nyingine mbili za VPL msimu huu, Ndanda FC na Mbeya City FC.
KAMPUNI ya Bin Slum Tyres imemaliza mkataba wake na klabu ya Stand United ya Shinyanga na klabu hiyo pekee Ligi Kuu kutoka mkoani humo msimu huu iko mbioni kuinhgia ubia na kampuni nyingine, imeelezwa.
Stand Utd na Ndanda FC zililamba udhamini wa mamilioni ya shilingi kutoka Bin Slum Tyres katika msimu wao wa kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Muhibu Kanu, mkurugenzi wa Stand Utd FC, ameuambia mtandao huu kuwa Bin Slum imeondoka katika klabu yao na watalamba udhamini mnono kutoka kwa kampuni nhyingine msimu ujao.
"Ni kweli Bin Slum ameondoka Stand United, Mungu akitusaidia tukabaki Ligi Kuu, msimu ujao tutalamaba udhamini mkubwa ambao utakuwa wa kihistoria katika klabu za soka Tanzania," amesema Kanu huku akisita kuitaja kampuni ambayo itamrithi Bin Slum.
Stand Utd inayonolewa na kocha mkuu Mganda Mathia Lule, ni miongoni mwa timu sita ambazo zinapambana kuhakikisha haziporomoki daraja kesho.
Timu nyingine ni Polisi Moro, Prisons, Ndanda FC, Mgambo Shooting na Ruvu Shooting.

0 comments:
Post a Comment