Friday, May 8, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
"Kagera haikuwa na upepo mzuri ilipohamishia maskani yake Mwanza msimu huu."
HALMASHAURI ya mji wa Bukoba Kagera, Kagera ililazimika kuufunga Uwanja wa Katiba ili kupisha ukarabati mkubwa unaodhaminiwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Uamuzi uliiathiri klabu ya Kagera Sugar ambayo ililazimika kusaka uwanja mwingine kwa ajili ya mechi zake za nyumbani katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Januari mwaka huu timu hiyo inayonolewa na kocha mkuu Mganda Jackson Mayanja akisaidiwa na mzawa Mrage Kabange, ilihamia jijini Mwanza.
Baada ya kuhamia jijini humo, timu hiyo ilipoteza mechi tatu mfululizo dhidi ya Azam FC, Mbeya City FC na Ndanda FC.
Vipigo hivyo vya mfululizo viliushtua uongozi wa wakatamiwa hao wa Kagera na kuamua kuihamishia timu mjini Shinyanga kuungana na Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Ikiwa mjini Shinyanga, Kagera Sugar FC ilifungwa mechi mbili tu dhidi ya Simba na wenyeji wa mji, Stand United.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sasa limeirudisha Kagera Sugar 'kuzimuni' CCM Kirumba jijini Mwanza ikacheze mechi ya mwisho msimu huu dhidi ya Tanzania Prisons FC kesho.
Mrage aliwahi kukaririwa akisema uwanja huo ni "mkubwa mno kwa kikosi chake."
Je, kikosi cha Mayanja kitaweza kufurukuta 'kuzimuni' kesho? Tusubiri tuone.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video