Friday, May 8, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Tanzania Prisons ni miongoni mwa timu tano ambazo zinapulia mashine kuukwepa mstari wa kuporomoka daraja msimu huu.'
KOCHA mkuu wa Tanzania Prisons, Mbwana Makatta, amesema kikosi cha wapinzani wao Kagera Sugar FC ni kizuri, lakini kesho hakitatoka salama jijini Mwanza.
Tanzania Prisons FC iliyoshinda 1-0 katika mechi iliyopita dhidi ya City jijini Mbeya, itakuwa na mtihani mgumu mbele ya Kagera Sugar FC wanaosaka nafasi ya nne, timu hizo zitakapochuana katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kesho jioni.
Katika mahojiano na mtandao huu kwa simu leo asubuhi akiwa Kanda ya Ziwa, Makatta amesema wanaiheshimu Kagera kutokana na ubora wa kikosi chake, lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi ya kesho ili waendelea kushiriki VPL.
"Kagera ni timu ngumu kutokana na kuwa na wachezaji wazuri na wenye nguvu, lakini kesho tunatakiwa kuwafunga. Ni ushindi tu utakaotuokoa kuporomoka daraja na hatuko tayari kwa hilo," ametamba Makatta.
Kocha huyo alikabidhiwa kukinoa kikosi cha Prisons baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo na kocha wa Simba 1999, David Mwamaja mzunguko wa pili.
Kagera imekusanya pointi 31 na itaingia uwanjani ikiwa haina hofu yoyote ya kuporomoka daraja, pengine itakuwa inasaka ushindi ili kupata zawadi ya mshindi wa nne.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video