Chacha akieleza kuhusu gazeti la dimba
Blog ya michezo ya Saleh Jembe imeripoti kwamba uongozi wa Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Tanzania Bara umetangaza kufungua kesi ya madai dhidi ya gazeti la Dimba ukitaka kulipwa fidia ya bilioni 3.
Yanga inataka kulipwa fedha hizo kufidia usumbufu mkubwa ilioupata baada ya gazeti hilo katika toleo lake la leo Aprili 29 namba ISSN 0856-2698 lililoandika kichwa kikubwa cha habari “Manji kufuru Yanga.”
Sehemu ya stori hiyo kubwa ilikuwa ikielezea uamuzi wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kutoa nyumba na magari kwa wachezaji wake.
Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha amezikanusha habari hizo na kusisitizi hakuna chochote kuhusiana na suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga jijini Dar es Saaam leo, Chacha amesema gazeti hilo limekuwa likiwanukuu vibaya au kunukuu ambacho hajasema viongozi wa klabu hiyo.
“Mara kadhaa, hali hii imekuwa ikitokea. Magazeti kadhaa ya nyuma pia yamefanya hivyo (alisema huku akionyesha baadhi ya magazeti ya Dimba).
“Hatuoni kama hili ni sahihi, hivyo pia tunawazuia Dimba kuandika habari zetu hadi hapo watakapoanza kuziandika kwa usafaha,” alisisitiza Chacha.
Hata hivyo, alisisitiza Yanga wanahitaji ushirikiano kutoka kwa vyombo vya habari huku akiamini kilichofanywa na Dimba hakikuwa sahihi na kinalenga kuvuruga umoja wa Yanga na Wanayanga kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment