Hans Poppe (kushoto) alimsajili Tambwe kutoka Vital'O ya Burundi
MWENYEKITI wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema klabu hiyo haijutii kumuacha mshambuliaji hatari wa Yanga, Amissi Tambwe katika dirisha dogo la usajili mwezi desemba mwaka jana.
Simba katika mazingira yasiyoeleweka waliamua kumuacha mfungaji huyo bora wa msimu uliopita dakika za mwisho za usajili na Yanga wakainasa saini yake kwa mkataba wa mwaka mmoja wakiamini anaweza kurudia magoli 19 aliyofunga msimu uliopita.
Kipindi anaachwa na Simba alikuwa ameifungia klabu hiyo goli moja tu, lakini sasa ana magoli 14, magoli matatu nyuma ya kinara Simon Msuva wa Yanga mwenye mabao 17 kilelen
Pia Tambwe amefunga 'hat-trick' mbili msimu huu akifuatiwa na Emmanuel Okwi na Ibrahim Hajibu waliofunga hat-trick moja moja.
"Hizi habari kwamba Simba inajutia kumuacha Tambwe (Amissi) nazishangaa, sisi hatuwezi kujutia kwasababu hakuwa na faida kwetu, alitufungia goli moja tu mpaka tunamuacha. Mwanzo alikuwa anaanza mechi, baadaye kocha (Patrick Phiri) akawa anampa dakika chache na kadiri siku zilivyoenda akawa anamuweka benchi kabisa, sasa tungeendelea kukaa na yeye kwa faida ipi?" Amehoji Hans Poppe.
Bosi huyo amesisitiza kuwa Tambwe ni mshambuliaji anayetegemea wachezaji wenzake wafanye kazi yeye amalizie tu na hawezi kufananishwa na Emmanuel Okwi.
"Tambwe anataka atafuniwe kila kitu ndio afunge, wachezaji wanaomtengenezea nafasi wakikabwa hawezi kufunga tena, lakini Okwi ni mchezaji anayehangaika, anafunga na kuwatengenezea wenzake nafasi".
Kauli hii inaweza kuwa ya kuzuga tu kutokana na ubora wa Tambwe kwa sasa kwasababu kiuchezaji amebadilika pia.
Anakaba na kupambana kutengeneza nafasi za kufunga.
0 comments:
Post a Comment