Uongozi wa timu ya Mbeya City Fc umetupilia mbali taarifa zilizoenea mtaani na kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna mpango wa kupanga matokeo kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara unaotarajia kuchezwa jumamosi kwenye uwanjani wa Sokoine dhidi ya Prison ya jijini hapa.
Akizungumza na kamati kuu ya uongozi wa mashabiki wa City jioni hii Katibu Mkuu wa Emmanuel Kimbe amesema hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya vilabu hivi viwili kuhusu mchezo wa jumamosi na ileweke wazi timu yao itaingia uwanjani kwa nguvu kusaka pointi tatu ambazo ni muhimu kwa ajili ya kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi.
“kwanza niseme wazi, nasikitishwa na taarifa hizi, katika hali ya kawaida huwezi kufanya jambo hilo hasa ukizingatia kupanga matokeo ni kosa na pili huwezi kupanga ufanya jambo hilo wakati unahitaji matokeo au pointi tatu ili ujiweke vizuri kwenye msimamo wa ligi, niwahaakikishia kuwa hakuna kubebana siku hiyo, timu ishinde kwa uwezo, tunahitaji sana pointi tatu za mchezo huo” alisema.
0 comments:
Post a Comment