Na George Mganga
Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia inatarajiwa
kuwasili Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya
mechi yao ya kukata na shoka dhidi ya Yanga
katika kombe la vilabu la Shirikisho barani
Afrika.
Habari kutoka Yanga zinasema wapinzani wao
wanaweza kutinga Dar es Salaam kati ya
Alhamisi au Ijumaa kwa mechi ya kwanza
itakayochezwa kati ya April 17 au 18 uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi ya marudiano itachezwa Tunis, Tunisia
baada ya wiki mbili.
Yaanza imeanza kuwavutia kasi wapinzani wao
kufuatia wimbi la ushindi katika mechi zake za
Ligi kuu.
Katika mechi za hivi karibuni, mabingwa hao wa
zamani waliweka historia ya mvua ya magoli
katika msimu baada kwa kuipa Coastal Union
kichapo cha 8-0 na baadae Mbeya City 3-1 na
kujikita kileleni ikiwa name pointi 46.
Tayari kocha wa Yanga, Hans Pluijm amewaonya
wachezaji wake kuwa makini na kuweka akilini
kuwa watakutana na moja ya timu ngumu barani
Afrika katika hatua ya 16 bora .
Yanga iliwatoa Wazimbabwe, Platinum FC na
sasa itatumia mechi zake za ligi kuu kama
sehemu ya mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo
muhimu.

0 comments:
Post a Comment