'Kaseja amewahi kuzidakia klabu kongwe nchini, Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).'
UONGOZI wa Stand United FC umesema mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu Stars ya Pwani ndiyo inayokwamisha usajili wa kipa mkongwe, Juma Kaseja, katika klabu hiyo ya Shinyanga.
Miezi miwili iliyopita Stand Utd kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Ufundi, Muhibu Kanu, iliweka wazi kufanya mazungumzo na Kaseja kuhusu kumsajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hata hivyo, katika mahoajino na mtandao huu leo akiwa Shinyanga, Kanu amesema mechi hiyo ndiyo kikwazo kikuu cha kufanyika kwa biashara hiyo.
"Mechi yetu dhidi ya JKT RUvu ndiyo itakayoamua hatma yetu kubaki Ligi Kuu ama kuporoka daraja, hivyo tumeamua kusubiri kwanza kabla ya kukamilisha usajili wa Kaseja.
"Huwezi kununua nguo ilhali mtoto bado hajazaliwa. Tunasubiri kuona atakuwa mtoto wa kike ama wa kiume," amesema Kanu.
Kaseja kwa sasa ana kesi dhidi ya Yanga SC iliyomfikisha mahakamani ikimdai zaidi mamilioni ya shilingi kwa madai ya kuvunja mkataba wake na klabu hiyo unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.


0 comments:
Post a Comment