WAPINZANI wa Yanga, Etoile du Sahel tayari wametua Dar es salaam alfajiri ya leo kuikabili Yanga kesho katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho itayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Etoile wanafanya mazoezi ya mwisho leo jioni uwanja wa Taifa wakati Yanga wao watakuwa uwanja wa Karume kujifua kwa mara ya mwisho.
Yanga wanahitaji kufunga magoli mengi ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Kuelekea katika mechi hiyo, kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi, Johannes Hans van der Pluijm amesema:
"Wachezaji wangu wapo katika hali nzuri kimchezo hakuna majeruhi . . Tunatambua kuwa tutakabiliana na mpinzani ambaye ana uzoefu mkubwa na historia nzuri kimafanikio lakini lazima utambue kuwa njia nzuri ya kushinda ni kutambua unachofanya na kujiamini,tumeangalia vizuri mbinu zao uwanjani naamini tutashinda mchezo wetu wa jumamosi,tutashambulia kila kona huku tukihakikisha hawatudhuru!mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuwashangilia vijana wetu"


0 comments:
Post a Comment