Friday, April 17, 2015

Daktari Hans Wilheim Muller Wohlfahrt ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha matibabu katika klabu ya Bayern Munich amejiuzulu kazi hiyo kufuatia kitengo chake hicho kulaumiwa baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Porto juzi jumatano katika mechi ya kwanza ya robo fainali klabu bingwa Ulaya
Timu hiyo imekuwa ikiandamwa na majeruhi hivi karibuni na katika mchezo iliwakosa Arjen Robben,Frank Ribery,David ,Javi Martinez na Mehdi Benatia ambao wote ni majeruhi.
Daktari huyo,72,ameamua kujiuzulu hapo jana baada ya kitengo chake matibabu kulaumiwa sana kwa madai ya kuwa majeruhi ndio chanzo cha kipigo hicho kutoka kwa Porto.
Kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola amekuwa na wasiwasi na kitengo hicho tangu mwanzoni mwa msimu huu kufuatia wachezaji wa timu hiyo kushindwa kupona haraka.
Bayer Munich itashuka dimbani wiki ijayo kuwakaribisha Porto katika mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali klabu bingwa Ulaya.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video