DIDIER Kavumbagu ni miongoni mwa washambuliaji wa kigeni wanaotokea kwenye 'Headline' za magazeti mengi ya michezo Tanzania, mitandao ya kijamii, redio na Televisheni.
Hii inatokana na umahiri wake wa kucheza soka na uwezo wa kucheka na nyavu.
Mpaka sasa Kavumbagu amefunga magoli 10 katika mechi 20 walizocheza na leo hii anaiongoza Azam fc kuchuana na Mgambo JKT uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Mtandao huu umepiga Stori na Kavumbagu na stori kubwa ilikuwa kuhusu wanawake wa Bongo wanavyowashobokea 'mastaa'.
Swali lilikuwa: Vipi Kavumbagu wanawake wanakusumbua sana wakitaka uwe mpenzi wao ili wakuchune 'Mihela' ya Bakhresa, wewe unachukuliaje hilo?
Kavumbagu anasema: "Wanawake wa Bongo wanasumbua sana, sio Bongo tu maeneo yote hasa unapokuwa maarufu. Wanapiga simu, wanatuma sms, picha wakihitaji mapenzi. Mimi najiuliza jambo moja tu, mbona wakati sina hela hawakuwepo? ninapata hela tu wanaanza kunisumbua".
"Cha msingi ni wewe mwenyewe kujipanga, mimi nina mke wangu na watoto, muda wa mapumziko napenda kukaa nyumbani na familia yangu, sipendi starehe. Nikiwa nyumbani napenda kusikiliza nyimbo nzuri, napenda muziki mzuri".
Swali la pili: Hukufunga dhidi ya Mbeya City fc na Mtibwa Sugar, bado una magoli 10, wakati Saimon Msuva mwenzako alifunga mawili dhidi ya Coastal Union ingawa hakufunga dhidi ya Mbeya City, ukame huu vipi tena?
Kavumbagu: aaaaah! kweli sijafunga, lakini mimi ni mshambuliaji ninayetaka kufunga muda wote na kuisaidia timu yangu. Leo tunacheza na Mgambo, nimejiandaa kufunga mungu akijaalia ili nimkute Msuva.
Tuna wenzetu majeruhi, daktari anafanya kazi ya ziada ili warudi, wachezaji tulibaki tumehamasishana kwamba leo lazima tushinde ili turejeshe matumaini ya kuchukua ubingwa tena.


0 comments:
Post a Comment