HII stori inatoka mechi ya ligi daraja la kwanza nchini Brazil 'Acreano Championship' ambapo Placido de Castro walifungwa magoli 5-2 na Rio Branco.
Baada ya kufungwa goli la tano kipindi cha pili, wachezaji wawili Uilian na Fábio Júnior wakaanza kunyosheana vidole na hatimaye kuanza kuzichapa ngumi kavukavu mithiri ya mabondi waliopo ulingoni.
Wachezaji wenzao wakawaamuria, lakini mwamuzi hakuwa na huruma, wachezaji hao wawili wa Placido de Castro walitolewa kwa kadi nyekundu.
Inawezekana wachezaji hao wamepigana kutokana na mzuka unaolizunguka pambano la Mayweather v Pacquiao litakalopigwa La vegas Marekani mei 2 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment