KOCHA wa zamani wa Tottenham na QPR, Harry Redknapp alikuwa mgeni katika 'shoo' ya TV ya Clare Balding na ameulizwa kuhusu kazi anayoiota kwasasa.
Kwa wakati huu ambao kocha huyo mkongwe mwenye miaka 68 hana kazi amekiri kupenda kufanya kazi Liverpool kwasababu ya sapoti na hali ya hewa ya klabuni hapo.
Redknapp amesema hali ya hewa ya Anfield inazifanya nywele zisimame nyuma ya shingo yako.
kocha wa sasa wa Liverpool, Brendan Rodgers yuko kwenye kiti cha moto, hivyo Redknapp anaweza kuwa mrithi wake kama anapewa nafasi.
0 comments:
Post a Comment