WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi ya mwishoni mwa wiki dhidi ya mabingwa wa msimu uliopita Azam fc.
Simba wapo chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) muda huu, lakini wameshindwa kuanza mazoezi mapema kutokana na mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na ikishakatika wanaingia kupasha kama kawaida.
"Tupo hapa chuo kikuu muda huu, tunasubiri mvua iishe ili tuanze mazoezi. Kila kitu kipo sawa, tunashukuru Mungu". Amesema Meneja wa Simba, Nico Nyagawa wakati akiongea na mtandao huu muda huu.
Simba wanajiandaa na mechi dhidi ya Azam itakayoamua hatima yao ya kushika nafasi ya pili.
Mpaka sasa Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 24, pointi nne nyuma ya Azam wanaoshika nafasi ya pili wakicheza mechi 23.
Mechi ya mwisho Simba watacheza na JKT Ruvu uwanja wa Taifa mei 9 mwaka huU.
0 comments:
Post a Comment