Kiungo mahiri wa Mbeya City Fc, Steven ‘Steve’ Mazanda anaweza kurejea dimbani wakati wowote kuanzia sasa kuendelea kuitumikia timu yake kufuatia kuimarika kwa afya yake iliyokuwa shakani baada ya kuumia goti akiwa mazoezini kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha ‘utabibu’ kwenye kikosi cha City, Dr Joshua Kaseko hali ya kiungo huyo inandelea kuimarika kwa kasi hivyo anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha City kwenye michezo miwili ya mwisho wa ligi msimu huu.
“Hali yake inaendelea kuimarika,amekuwa na mapumziko ya majuma zaidi ya matatu sasa,imani yangu kuwa atarejea kucheza kwenye michezo miwili ya mwisho” alisema.
Mazanda aliumia goti mazoezini uwanja wa Sokoine wakati City ikijiandaa kuivaa Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Kwa upande mwingine Dr Kaseko amedokeza kuwa mlinzi Yufuph Abdalah Sisalo anatarajia kurejea dimbani kwenye mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar wikiendi ijayo kufuatia kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.
Sisalo aliyefunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliochezwa jijini Dar, aliumia goti la mguu wa kulia wakati City ikicheza na Ndanda Fc kwenye uwanja wa Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara.
“Sisalo yuko vizuri sasa, huyu hapa nadhani unamuona anafanya mazoezi mepesi, nitamtizamia kesho ingawa nina uhakika atarejea uwanjani kucheza mchezo ujao”.
0 comments:
Post a Comment