TIMU ya taifa ya soka ya wanawake nchini, Twiga Stars leo imefanikiwa kufuzu Michuano ya Afrika mara baada ya kuiondoa Zambia almaarufu She-Polopolo kwa jumla ya mabao 6-5.
Twiga ambayo ipo chini ya mkufunzi Rogasian Kaijage jioni ya leo ilikiwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ambapo imejikuta ikilala mbele ya wanawake hao kutoka Zambia kwa jumla ya mabao 3-2.
Hata hivyo bahati pekee iliyowakuta wanadada hao wa Tanzania ni kutokana mchezo wa awali kushinda nchini Zambia kwa mabao 4-2.
Kwa upande wa Twiga leo mabao yao yalifungwa na Asha Rashid 'Mwalala' dakika ya tatu na Mwanahamisi Chiuwa 'Gaucho' dakika ya 29, huku Zambia wakijipatia mabao yao kupitia kwa Grace Chanda dakika ya 50, Irene Lungu dakika ya 61 kwa mkwaju wa penalti mara baada ya Nahodha Sofia Mwasikili kuunawa mpira katika eneo la hatari huku la tatu na la ushindi likiwekwa kimiani na Misozi Chisa mnamo dakika ya 90.
Kwa mantiki hiyo sasa Twiga itakwenda Kongo ya Brazavile Septemba mwaka huu kwa ajili ya AAG.

0 comments:
Post a Comment