MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi akiongea na waandishi wa habari leo walipotembelea akademi ya Slivester Marsh jijini Mwanza.
TIMU ya Simba leo asubuhi majira ya saa nne imetembelea kituo cha kukuza na kulea vipaji 'akademi' ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, Marehemu, Slivester Marsh na kutoa fursa kwa wachezaji wake na makocha kuongea na vijana wanaolelewa na kituo hicho.
Pia Simba imetoa rambirambi na kukisaidia kituo hicho vifaa mbalimbali vya michezo.
Msemaji wa Simba, Hajji Manara ameuambia mtandao huu kuwa wataendelea kufanya shughuli za kijamii pindi wapatapo fursa.








0 comments:
Post a Comment