Friday, April 10, 2015

Chelsea wapo mbioni kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kabisa nchini Uingereza kuchukua ubingwa huku ikiwa imekaa kileleni kwa muda merefu zaidi.
Vijana hao wa London waliopo chini ya kocha Jose Mourinho walianza kuongoza ligi tangu walipoifunga Everton mnamo tarehe 30, August kwa idadi ya magoli 6-3 baada ya michezo miwili tu tangu ligi kuanza, huku Tottenham wakiongoza kabla ya hapo. 

Chelsea wamekuwa kileleni kwa takribani siku 230 mpaka sasa, japo kwa wakati fulani walilingana kwa kila kitu na timu ya Manchester City.
 Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea mara baada ya kuifunga timu ya Stoke City kwa magoli 2-1, katika mchezo uliochezwa Jumamosi iliyopita.



 
Steve Bruce (kushoto) na Bryan Robson wakiwa wamebeba kombe baada ya timu yao ya Manchester United kukaa kileleni kwa takribani siku 262 katika msimu wa ligi wa mwaka1993/94
Hizi ndizo Timu zilizoongoza kukaa kileleni kwa muda mrefu
Manchester United 1993/94 - 262
Chelsea 2005/06 -257
Man Utd 2006/07 -250
Man Utd 2000/01 -241
Chelsea 2014/15 - 230*
Arsenal 2003/04 - 216
Newcastle 1995/96 -212
Chelsea 2009/10 - 204
Chelsea 2004/05 - 193
Man Utd 2012/13 -191

*Mpaka sasa
Mpaka sasa Man U ndiyo wanashikilia rekodi hiyo baada ya kutwaa ubingwa mwaka 
1993/94 wakiwa chini ya Sir Alex Ferguson huku wakikaa kileleni kwa siku 262.
Lakini hata hivyo Chelsea wanaweza kuipita rekodi hii ndani ya siku 12 zijazo au endapo watakaa mpaka mwisho wa msimu huu.
Chelsea waliikaribia rekodi hii msimu wa 2005/06 wakati wakiwa chini ya huyuhuyu Mourinho walipokaa kileleni kwa takribani siku 257 wakati Man U walikaa siku 250 na 241 katika msimu wa 
2006/07 na 2000/01.

Arsenal ambayo ilimaliza msimu wa mwaka 2003/04 bila ya kufungwa waliongoza ligi kwa siku 216.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video