Thursday, April 16, 2015

John Tegete


Na Kassim Mtolea, Mwanza

KOCHA mkuu wa Wanakishamapanda timu ya Toto Africans ya Mwanza,  John Tegete ameonesha kuvutiwa na kiungo wa wekundu wa Msimbazi Simba.
Hali hiyo ilijitokeza siku ya pambano la kirafiki lililokuwa maalum kwa kuipongeza timu ya Toto  kupanda ligi kuu msimu ujao kwenye dimba la CCM Kirumba jijini hapa.
Tegete alisikika akisema waziwazi kuwa lazima amtwae kijana huyo"Huyu mtoto aliyevaa jezi namba ishirini na saba lazima nimpate  kwa hali na mali ili aje kunisaidia"alisema Tegete, akimaanisha kiungo Abdallah Seseme.
Mara baada ya pambano hilo mchezaji huyo aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili cha Simba alikutwa akiwa kwenye benchi la timu ya Toto akimsubiri kocha wa timu hiyo aliyekuwa anaongea na wanahabari uwanjani hapo.
Baada ya kuachana na wanahabari kocha huyo alikutana na Seseme,huku Seseme akionekana kutoa namba kwa haraka kwa mwalimu huyo na hatimaye kukimbilia kwenye basi la timu ambalo lilikuwa tayari linaanza safari.
Mchezaji huyo amekuwa hana uhakika kucheza kwenye kikosi cha wekundu wa msimbazi hivyo kutajwa kuachana na timu mara tu kandarasi yake itakapo malizika mwishoni mwa msimu huu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video