Na Kassim Mtolea, Mwanza
Baada ya kipa wa Toto African ya Mwanza, Erick Ngwengwe kutangaza kuipa mkono wa kwaheri timu hiyo itakayo shiriki ligi kuu msimu ujao, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kusema upo tayari kukaa faragha na mlinda lango huyo ili kumalizana naye.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Waziri Ahmed Gao amezungumza na MPENJA BLOG na kukiri kuwepo kwa taarifa hizo na amesisitiza wapo tayari kuketi na mchezaji huyo ili kufikia makubaliano.
"Erick ni kama mtoto wangu na nimekaa naye hapa kwa amani kwahiyo naamini atanielewa na huenda akabaki tena hapa msimu ujao"alisema makamu mwenyeki.
Gao alisema kuwa kweli kipa huyo haridhishwi na hali ya mambo kwenye timu hiyo kutokana na kukoekana kwa umoja na ushirikiano miongoni mwa viongozi wa timu hiyo.


0 comments:
Post a Comment