YANGA SC baada ya sare ya 1-1 na Etoile du Sahel waliyoambulia mwishoni mwa juma lililopita uwanja wa Taifa mechi ya kwanza hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho kesho wataivaa Stand United katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro ametamba kuwa wazee wa kimataifa ,wazee wa dozi wamerejea kuleta dozi ambayo mashabiki wameikosa, kwahiyo Stand wajipange kupokea kipigo kizito.
Baada ya kusikia maneno hayo, Mkurugenzi wa ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu amejibu kuwa Yanga wajipange na wasitarajie mtelemko kesho kwani timu ni nyingine kabisa na ile waliyoifunga magoli matatu Shinyanga.
"Leo jioni tumefanya mazoezi uwanja wan Karume, tuko tayari kukabiliana na Yanga, tunaiheshimu Yanga, lakini tumejianda kivingine kabisa," Amesema Kanu na kuongeza: "Ni kweli walitufunga magoli matatu Shinyanga, ukiangalia Stand ni timu iliyoanza juzi tu, Yanga ni timu ya miaka mingi, tumejipanga sasa, Yanga waje vizuri, tumekuwa na kikosi chenye wachezaji ambao hawakuwaona kama Chanongo, Chidiebele na wengine".
Kuhusu Yanga kuwa tishio, Kanu amejibu: "Ameongezeka Sherman (Kpah) peke yake, wote wanakabika, beki wangu atakumkaba vilivyo, tutampa majukumu nahodha Peter Mutabuzi kwa ajili ya kuhakikisha kazi ya kumbaka Sherman inakamilika"


0 comments:
Post a Comment