Mshambulizi
wa Nigeria Odion Ighalo, amefananisha mechi mbili za Watford
zilizosalia za ligi daraja ya pili na fainali, huku klabu hiyo
ikikaribia kufuzu kwa ligi kuu ya Premier nchini Uingereza.
Watford inaongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa alama
moja, huku ikiwa imesalia na mechi moja ya ugenini dhidi ya Brighton na
nyingine dhidi ya Sheffield Wednesday katika uwanja wao wa nyumbani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amesema wameafikia
matokeo hayo kwa sababu ya nia, ila amesisitiza kuwa ni sharti washinde
mechi hizo zilizosalia.
''Tayari tunayo tiketi ya kupandishwa daraja na kamwe hatuwezi kupoteza nafasi ya kuandikisha historia'' Alisema Ighalo.
Ushindi wao wa bao moja kwa bila dhidi ya Birmingham siku
ya Jumamosi ilifufua matumaini ya Watford, na kuweka katika nafasi nzuri
kuliko Bournemouth, ambayo inashikilia nafasi ya pili sawa na
Middlesbrough lakini inadumishwa na idadi ya magoli.
Msimu wa mwaka wa 2012/13, Watford ilipoteza nafasi ya
kupanda daraja baada ya kushindwa na Cyrstal Palace katika hatua ya
muondoano.


0 comments:
Post a Comment