KOCHA wa Mgambo JKT, Bakari Shime amekiri kusikia tetesi za mabingwa mara 24 wa ligi kuu Tanzania bara, Dar Young Africans kuitaka saini ya mshambuliaji wake nyota, Malim Francis Busungu.
Busungu ni mshambuliaji hatari na mpaka sasa amefunga magoli 9 sawa na Amissi Tambwe wa Yanga na Abasirim Chidiebele wa Stand United.
Anazidiwa magoli manne tu na kinara wa ufungaji Simon Msuva mwenye magoli 13 kileleni akifuatiwa na Didier Kavumbagu wa Azam fc na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar wenye magoli 10 mpaka sasa.
Shime amesema: "Nimezisikia tetesi za Yanga kumhitaji mshambuliaji wangu Busungu (Malim), lakini nimemwambia (Busungu) afanye kazi, aachane na maneno hayo kwa wakati huu".
Mbali na Yanga, Simba nao wanahusishwa kutaka kumsajili nyota huyo.
Kuhusu mechi ya keshokutwa dhidi ya Simba uwanja wa Taifa, Shime amesema wapo tayari kuchuana kusaka pointi tatu.
"Simba wametoka kufungwa Mbeya, wana hasira, lakini hapa sio sehemu sahihi ya kupunguza machungu, tuko barabara na bahati mbaya sijawahi kuziogopa Simba na Yanga". Amesema Shime.
0 comments:
Post a Comment